Roll-Up Banners: Chagua Vizuri, Vutia Zaidi
Roll-up banner ni moja ya zana bora zaidi za uuzaji wa ana kwa ana — rahisi kubeba, haraka kusimamisha, na inaweza kuvutia macho kwa urahisi.
Aina za Roll-Up Banners
Broadbase (Msingi Pana): Inasimama imara zaidi. Inafaa kwa matumizi ya ndani — ofisi, maonyesho, maduka. Saizi: 85cm × 200cm.
Smallbase (Msingi Mdogo): Nyepesi zaidi na rahisi kubeba. Inafaa kwa matumizi ya dharura au safari.
Msingi wa Chuma au Plastiki?
Chuma ni imara zaidi, inafaa kwa matumizi ya mara kwa mara. Plastiki ni mwepesi na bei nafuu lakini inaweza kuvunjika. Kama unatumia mara nyingi kwa mwezi — chagua chuma.
Muundo Bora wa Banner
Watu hawasimami kusoma — wanaangalia kwa sekunde 3. Ujumbe mmoja mkuu, fonti kubwa, logo inayoonekana, na nambari ya simu au WhatsApp.
DP Promotions inachapisha roll-up banners za ubora wa juu — design, print na delivery. Piga simu: +255 711 800 400.