Sera ya Faragha
Imesasishwa: Novemba 2026
1. Taarifa tunazokusanya
Tunakusanya taarifa unazotupatia moja kwa moja, jina, namba ya simu, barua pepe na maelezo ya project, pale unapojaza fomu, kupiga simu, au kuwasiliana nasi kupitia WhatsApp au portal yetu.
2. Jinsi tunavyotumia taarifa
Tunatumia taarifa zako kukupatia huduma, kuandaa quotation, kuwasiliana kuhusu order yako, na (ukikubali) kukutumia ofa na elimu ya branding kupitia mailing list yetu.
3. Google Analytics, Meta Pixel na Cookies
Tovuti hii hutumia Google Analytics na Meta Pixel kuelewa jinsi wageni wanavyotumia tovuti na kupima matangazo yetu. Zana hizi huwashwa tu baada ya wewe kubonyeza "Kubali" kwenye taarifa ya cookies. Ukibonyeza "Kataa", hazihifadhi cookies za takwimu wala za matangazo. Unaweza kubadilisha uamuzi wako kwa kufuta cookies na data ya tovuti hii kwenye browser yako.
4. Kushiriki taarifa
Hatuuzi wala kukodisha taarifa zako kwa wahusika wengine. Tunazishiriki tu pale inapohitajika kisheria au kukamilisha huduma uliyoomba.
5. Haki zako
Una haki ya kuomba kuona, kurekebisha, au kufuta taarifa zako wakati wowote. Wasiliana nasi kupitia sales@dppromotions.co.tz.
6. Mawasiliano
Kwa maswali kuhusu privacy, tuandikie: sales@dppromotions.co.tz au piga +255 711 800 400.