QR code moja kwenye kipeperushi, kadi ya biashara au bango inaweza kukutumikia kwa miaka, hata namba yako, ofisi yako au ofa zako zikibadilika. Mwongozo huu unaeleza dynamic QR inavyofanya kazi, mahali pa kuiweka, na kadi za NFC zinazoibeba kwa kugusa simu.
Kwa ufupi
- QR ya kawaida (static) inafungia taarifa ndani yake. Ikichapishwa, haibadiliki tena.
- Dynamic QR inabeba kiungo (link) kisichobadilika kinachoelekeza kwenye ukurasa wako. Unabadilisha ukurasa, QR iliyochapishwa inabaki ile ile.
- Unaichapisha kwenye vitu unavyochapisha tayari: kadi za biashara za karatasi, vipeperushi, brosha, mabango, magari na vifungashio.
- Kadi ya NFC ni kadi ya plastiki iliyochapishwa yenye chip na QR ile ile. Mteja anagusa simu au anascan, na zote zinafungua ukurasa mmoja.
- Kila mara kadi yako inapofunguliwa, kwa QR, NFC au kiungo, inahesabiwa, hivyo unaona kama unachochapisha kinaleta wateja. Unaweza kuanza bure kwenye card.dppromotions.co.tz.
Mwezi Desemba ulichapisha vipeperushi (flyers) elfu mbili vya ofa ya msimu. Kila kipeperushi kilikuwa na QR code iliyompeleka mteja kwenye bei za ofa. Januari ofa imekwisha, lakini vipeperushi bado viko kwenye mbao za matangazo, kwenye maduka ya marafiki, na ndani ya mabegi ya wateja. Kila anayescan leo anaona bei ambazo hazipo tena. Hana sababu ya kukupigia, na wewe hujui kama alicheka au alikasirika.
Hiki ni kikwazo ambacho biashara nyingi zinakutana nacho bila kukitambua. QR code imekuwa kawaida kwenye kila kitu kinachochapishwa Tanzania: kadi za biashara, vipeperushi, menyu za migahawa, mabango ya maduka, magari ya kampuni. Lakini QR nyingi zinazochapishwa ni za aina moja: zile zinazofungia taarifa ndani yake. Zikishachapishwa, zimekwisha. Taarifa zikibadilika, QR inakuwa uongo uliochapishwa kwa rangi nzuri.
Makala hii inakupitisha hatua kwa hatua. Kwanza tunaangalia kwa nini QR iliyochapishwa inazeeka haraka na inakugharimu kiasi gani. Kisha tunaeleza dynamic QR, QR inayobaki ile ile huku taarifa nyuma yake zikibadilika, na jinsi inavyokaa vizuri kwenye vitu unavyochapisha tayari. Tunaeleza pia kadi za NFC, ambazo ni kadi za biashara za plastiki zinazobeba QR hiyo hiyo pamoja na uwezo wa kugusa simu. Mwisho tunakupa hatua saba za kuanza wiki hii.
01QR iliyochapishwa isiyoweza kubadilika
Ili kuelewa tatizo, inasaidia kujua QR ya kawaida inafanya nini hasa. QR ni picha inayobeba maandishi. Maandishi hayo yanaweza kuwa namba ya simu, kadi ya mawasiliano (vCard), au kiungo (link) cha tovuti. Kwenye QR ya kawaida, maarufu kama static QR, maandishi hayo yamefungiwa ndani ya picha yenyewe. Kubadilisha herufi moja kunamaanisha kutengeneza picha mpya kabisa, na kwa kitu kilichochapishwa, kuchapisha upya.
Kampuni Yako Ltd
Kadi za biashara: taarifa za mwaka jana
Wengi huweka vCard kwenye QR ya kadi ya biashara, ili mteja ascan na kukuhifadhi moja kwa moja. Ni wazo zuri hadi siku namba inapobadilika. Sisi wenyewe tulipitia hili: ofisi ya DP Promotions ilihama kutoka Tabata Kisukuru kwenda Mtaa wa Mlando, Ilala. Kila kadi yenye anwani au QR ya zamani iliyokuwa mikononi mwa wateja ilianza kuwapeleka mahali pasipo sahihi, na hakuna njia ya kuzirudisha.
Vipeperushi na brosha: ofa zilizokwisha
Kipeperushi kinaishi muda mrefu kuliko ofa iliyokibeba. Kinabandikwa ukutani, kinawekwa kwenye droo, kinapitishwa kwa mtu mwingine. QR iliyompeleka mteja kwenye bei za Desemba itaendelea kufanya hivyo hadi Juni. Kila anayescan baadaye ni mteja mwenye nia anayekutana na taarifa zisizo sahihi.
Mabango, magari na vifungashio: gharama kubwa kubadilisha
Kadi ya biashara ni rahisi kuchapisha upya. Bango la duka, stika ya gari au mzigo wa vifungashio si rahisi hivyo. Kama QR kwenye bango la mita tatu inaelekeza kwenye tovuti iliyobadilisha anwani, unalazimika kuchagua kati ya kuchapisha bango jipya au kuacha QR isiyofanya kazi ikitazamwa na kila anayepita.
Hujui kama inafanya kazi
Ulichapisha vipeperushi elfu mbili. Ni vingapi kati ya hivyo viliscaniwa? Ni eneo gani lilileta wateja wengi zaidi, Kariakoo au Mlimani City? Bango la dukani lina nguvu kuliko stika ya gari? Static QR haiwezi kujibu swali lolote kati ya haya. Unaendelea kuchapisha kwa kukisia.
02Gharama zinazojificha
Gharama ya QR ya kawaida haiko kwenye kuitengeneza, kwa sababu kuitengeneza ni bure. Iko kwenye kile kinachotokea baadaye.
- Kuchapisha upya: kila badiliko la namba, anwani, tovuti au bei linamaanisha kadi mpya, vipeperushi vipya, na wakati mwingine bango jipya.
- Wateja wanaopotea kimya kimya: mteja anayescan na kukuta taarifa za zamani hakupigii simu kukuambia. Anaenda kwa mwingine.
- Mfanyakazi anayeondoka: kadi zenye QR ya namba yake binafsi zinaendelea kumpelekea wateja wa kampuni hata baada ya kuondoka.
- QR zilizokufa: baadhi ya tovuti za bure za kutengeneza QR zinatoa QR inayokufa baada ya muda, au inayoonyesha matangazo ya kampuni nyingine kabla ya ukurasa wako. Siku inapokufa, kila kitu ulichochapisha kinakuwa bure.
- Matumizi ya kukisia: bila takwimu, bajeti ya uchapishaji inagawanywa kwa mazoea badala ya matokeo.
03QR na NFC ni nini? Kwa lugha rahisi
Kabla ya kuendelea, tuelewe teknolojia mbili zinazotumika hapa. Zote mbili zina kazi moja: kumfikisha mteja kwenye ukurasa wako bila kuandika chochote.
QR code: picha inayosomwa na kamera
QR code ni ile picha ya miraba midogo myeusi na myeupe unayoiona kwenye vifungashio, menyu na mabango. Ifikirie kama barcode iliyo kwenye bidhaa dukani, lakini badala ya kubeba bei, inabeba kiungo au maandishi.
Inavyofanya kazi: mteja anafungua kamera ya simu na kuielekeza kwenye QR. Kamera inasoma miraba ile, inaigeuza kuwa kiungo, na kumuonyesha kitufe cha kufungua. Anabonyeza, ukurasa unafunguka. Hakuna app ya ziada kwa simu nyingi za kisasa.
Inahitaji nini: simu yenye kamera na mtandao. Inachapishwa kwenye kitu chochote: karatasi, plastiki, kitambaa, bango au stika.
NFC: kugusa kunakofungua ukurasa
NFC ni kifupi cha Near Field Communication, yaani mawasiliano ya karibu sana. Ni teknolojia ile ile inayotumika unapolipa kwa kugusa kadi ya benki kwenye mashine, au kugusa kadi kwenye geti la mwendokasi.
Inavyofanya kazi: ndani ya kadi kuna chip ndogo na antena nyembamba, na haina betri. Simu yenye NFC ikiikaribia kwa sentimita chache, simu inaipa chip nguvu kidogo ya kutosha kusoma kiungo kilichohifadhiwa ndani yake. Ukurasa unafunguka papo hapo, bila kufungua kamera.
Inahitaji nini: simu yenye NFC iliyowashwa. Simu nyingi za kisasa za Android na iPhone zinayo. Kwa simu zisizo nayo, QR iliyo nyuma ya kadi ile ile inafanya kazi.
04Dynamic QR inavyofanya kazi
Dynamic QR inatatua tatizo kwa njia rahisi. Badala ya kufungia taarifa zako ndani ya picha, QR inabeba kiungo kifupi kisichobadilika, kwa mfano card.dppromotions.co.tz/jina-lako. Kiungo hicho kinaelekeza kwenye ukurasa wako mtandaoni. Kwenye DP Card, ukurasa huu ndio kadi yako ya kidigitali. Taarifa zinakaa kwenye ukurasa, si kwenye QR.
Matokeo yake ni haya: QR uliyochapisha leo haitabadilika kamwe, lakini kile mteja anachokiona akiiscan kinabadilika kila unapohariri ukurasa. Namba mpya, anwani mpya, orodha mpya ya bei, picha za kazi mpya: unaingia kwenye dashibodi, unabadilisha, unahifadhi. Sekunde hiyo hiyo, kila kipeperushi, kadi na bango lenye QR hiyo kinaonyesha taarifa mpya.
Static QR na dynamic QR: tofauti zake
| Kipengele | Static QR | Dynamic QR |
|---|---|---|
| Kubadilisha taarifa | Haiwezekani bila kuchapisha upya | Wakati wowote, QR inabaki ile ile |
| Kupima matokeo | Haiwezekani | Kila mara kadi inapofunguliwa inahesabiwa |
| Ukubwa wa QR | Inajaa zaidi kadiri taarifa zinavyoongezeka | Ndogo na safi, kwa sababu inabeba kiungo kifupi tu |
| Mfanyakazi akiondoka | Kadi zake zinaendelea kumpelekea wateja | Ukurasa unahamishiwa kwa mtu mwingine |
| Mteja anachokiona akiscan | Maandishi au namba tu | Ukurasa kamili: simu, WhatsApp, ramani, picha, orodha ya bei |
Mteja anaona nini akiscan
Kwenye DP Card, QR inampeleka mteja kwenye ukurasa mwepesi uliopangwa kwa simu. Kila taarifa ni kitufe: kubonyeza namba kunapiga simu, kubonyeza WhatsApp kunafungua mazungumzo bila kuhifadhi namba kwanza, kubonyeza anwani kunafungua ramani hadi mlangoni, na kitufe cha "Hifadhi namba" kinakuweka kwenye orodha ya mawasiliano ya simu yake kwa kubonyeza mara moja. Unaweza pia kuongeza huduma na bei, hadi picha sita za kazi zako, hadi nyaraka nne za PDF kama wasifu wa kampuni (company profile) au orodha ya bei, fomu ya mteja kuacha ombi, na saa za kazi.
Hakuna app ya kupakua. Kamera ya simu inascan, ukurasa unafunguka kwenye browser ya iPhone au Android. Ukurasa wote una uzito wa chini ya KB 70, hivyo unafunguka haraka hata kwenye mtandao dhaifu na haimalizi bando la mteja.
Ukurasa unaweza kuvaa muonekano wa chapa yako. DP Card ina miundo 20, na rangi ya chapa yako inawekwa kwenye muundo wowote.
Ukurasa mmoja, matumizi mengi
Kwa sababu ukurasa unabadilika, QR moja inaweza kufanya kazi tofauti kwa nyakati tofauti. Desemba inaonyesha ofa ya msimu kwenye maelezo na orodha ya bei ya PDF. Januari unabadilisha PDF kuwa orodha ya kawaida ya bei. Ukihamia ofisi mpya, unabadilisha anwani. Vipeperushi vile vile vinaendelea kufanya kazi muda wote huo.
05Mahali pa kuiweka: vitu unavyochapisha tayari
Faida kubwa ya dynamic QR ni kwamba haikutaki uache ulichozoea. Bado unachapisha kadi za biashara, bado unagawa vipeperushi, bado una bango la dukani. Tofauti ni kwamba sasa kila kimoja kina mlango unaoelekeza kwenye taarifa sahihi za leo.
Kadi za biashara za karatasi
Weka QR upande wa nyuma au kona ya mbele. Mteja anasoma jina lako kwa macho, kisha anascan kukuhifadhi. Kadi uliyochapisha leo itabaki sahihi hata ukibadilisha namba mwakani. Tazama mfano kwenye video yetu fupi ya kadi ya pande mbili yenye QR.
Vipeperushi na brosha
Weka QR karibu na mwito wa kuchukua hatua, kwa mfano "Scan kuona bei" au "Scan kuagiza kwa WhatsApp". Ofa ikiisha, badilisha ukurasa badala ya kutupa vipeperushi vilivyobaki.
Mabango ya duka na ofisi
Mpita njia anayeona bango saa nne usiku, duka likiwa limefungwa, anascan, anaona saa za kazi na ramani, na anaacha ombi kwenye fomu.
Magari ya kampuni
Gari ni bango linalotembea. QR kubwa ya kutosha kwenye mlango wa nyuma inaonekana kwenye foleni, mahali ambapo watu wana muda wa kuscan.
Roll-up banners na mabanda ya maonyesho
Kwenye Sabasaba au maonyesho mengine, wageni wengi hawana muda wa kuongea. QR inawaruhusu kuchukua mawasiliano yako na kuondoka, kisha kukutafuta baadaye.
Vifungashio, risiti na ankara
Mteja aliyekwisha kununua ndiye anayeweza kurudi. QR kwenye mfuko, kifungashio au risiti inamrudisha kwako akihitaji tena.
DP Promotions inachapisha vitu hivi vyote: kadi za biashara, vipeperushi, brosha, roll-up banners, mabango, stika za magari na vifungashio. Ukiagiza uchapishaji kwetu, tunaweka dynamic QR yako kwenye muundo kabla ya kuchapisha, kwa ukubwa na nafasi inayoscaniwa kwa urahisi.
06Kadi ya NFC: QR ile ile, pamoja na kugusa
Hapa ndipo watu wengi huchanganyikiwa, kwa hiyo tuiweke wazi. Dynamic QR ni msingi. Kadi ya biashara ya kidigitali ya NFC si bidhaa tofauti; ni njia nyingine ya kubeba QR hiyo hiyo.
Dynamic QR na ukurasa wako
Kiungo kimoja kisichobadilika na ukurasa wa taarifa zako. Unaubadilisha wakati wowote.
Kadi za karatasi, vipeperushi, mabango
QR ile ile inachapishwa kwenye kila kitu unachogawa au kubandika.
Kadi ya NFC ya plastiki
Kadi iliyochapishwa yenye chip ya NFC na QR ile ile nyuma. Kugusa au kuscan.
Kadi ya NFC ni kadi ya plastiki ya ukubwa wa kadi ya benki (85.6 x 54 mm), iliyochapishwa kwa nembo na rangi za kampuni yako. Ndani yake kuna chip ndogo ya NFC iliyounganishwa na kiungo cha ukurasa wako. Nyuma yake imechapishwa QR ile ile. Mteja anaweza kufungua ukurasa wako kwa njia mbili kutoka kadi moja:
- Kugusa: anagusa kadi nyuma ya simu yenye NFC, ukurasa unafunguka papo hapo.
- Kuscan: kama simu yake haina NFC, au NFC imezimwa, anascan QR iliyo nyuma ya kadi.

Kampuni yako
Kampuni yako
DP Card kwa vitendo: gusa, scan, badilisha
Sekunde 58 zinazoonyesha kadi ya NFC ikigusa simu, QR ikiscaniwa, na taarifa zikibadilishwa bila kuchapisha upya.
Tazama YouTubeKadi ya karatasi au ya NFC: ipi uchague?
Si lazima uchague moja. Kadi za karatasi zenye dynamic QR ni za kugawa kwa wingi: maonyesho, semina, wateja wanaopita. Kadi ya NFC ni ya kubaki mkononi mwako. Unaigusa kwenye simu ya mteja, ukurasa unafunguka, mteja anakuhifadhi, na kadi inarudi mfukoni. Kadi moja ya NFC inaweza kukutumikia kwa miaka, wakati kadi za karatasi zinaisha na kuchapishwa tena.
Kwa kawaida tunashauri mchanganyiko huu: kadi ya NFC kwa mameneja na wafanyakazi wa mauzo wanaokutana na wateja ana kwa ana, na kadi za karatasi zenye QR kwa kugawa kwenye matukio makubwa. Zote zinaelekeza kwenye ukurasa mmoja, kwa hiyo mteja anapata taarifa zile zile popote alipokupata.
07Kwa kampuni: QR na kadi kwa kila mfanyakazi
Kwa kampuni, dynamic QR inaleta udhibiti ambao karatasi haiwezi kutoa.
Kuweka timu nzima kwa faili moja
Unapakia faili la Excel lenye majina, vyeo, namba na email za wafanyakazi. Kila mmoja anapata ukurasa wake na QR yake, zote zikiwa na muonekano mmoja wa chapa ya kampuni. QR hizo zinachapishwa kwenye kadi za karatasi au kadi za NFC za kila mfanyakazi.
Mfanyakazi akiondoka, wateja wanabaki
Ukurasa wa mfanyakazi aliyeondoka unazimwa au unahamishiwa kwa anayechukua nafasi yake. Kadi zote na vipeperushi vyenye QR yake vinaendelea kufanya kazi, lakini sasa vinampeleka mteja kwa mtu sahihi. Wateja wa kampuni wanabaki kuwa wa kampuni.
Takwimu za kila kadi
Kila ukurasa una takwimu zake. Unaona kitengo kipi au tawi lipi linafikia wateja wengi, na tukio gani la maonyesho lilileta mawasiliano mengi.
Mara zilizofunguliwa, siku 30 Takwimu za mfano
Kwa vifurushi vya Business na Enterprise, kampuni inaweza kutumia jina lake la tovuti (domain), kwa mfano card.kampuniyako.co.tz, ili hata kiungo kilicho ndani ya QR kibebe jina la kampuni. Kadi zote zinafunguka kupitia HTTPS, na taarifa ni mali ya kampuni.
Siku moja ya QR moja: mfano wa vitendo
Neema ni meneja wa mauzo wa kampuni ya kusambaza vifaa vya usafi Dar es Salaam. Kampuni yake ilichapisha vipeperushi, kadi za karatasi na stika za magari, zote zikiwa na dynamic QR, na Neema ana kadi ya NFC.
Saa 2 asubuhi. Neema anabadilisha orodha ya bei ya PDF kwenye ukurasa wake kwa sababu bei za mzigo mpya zimefika. Vipeperushi vilivyogawiwa wiki iliyopita sasa vinaonyesha bei mpya.
Saa 4 asubuhi. Anatembelea hoteli mpya Masaki. Anagusa kadi yake ya NFC kwenye simu ya meneja wa hoteli. Meneja anabonyeza "Hifadhi namba" na kupakua wasifu wa kampuni kabla mazungumzo hayajaisha.
Saa 7 mchana. Mteja wa zamani anascan QR kwenye kadi ya karatasi ya afisa aliyeondoka mwezi uliopita. Kwa sababu ukurasa ule ulihamishiwa kwa Neema, mteja anafika moja kwa moja kwake.
Saa 10 jioni. Dereva aliye kwenye foleni nyuma ya gari la kampuni anascan stika ya QR na kuacha ombi la quotation kwenye fomu.
Mwisho wa mwezi. Takwimu zinaonyesha kuwa kadi ya timu ya Kariakoo inafunguliwa mara nyingi kuliko za matawi mengine. Bajeti ya uchapishaji ya mwezi ujao inaelekezwa huko.
08Hatua 7 za kuanza wiki hii
Tengeneza ukurasa wako bure
Fungua card.dppromotions.co.tz, jisajili kwa akaunti ya Google, jaza simu, WhatsApp, email, tovuti, anwani na saa za kazi. Chagua muundo (template) unaoendana na chapa yako. Ndani ya dakika tano una kiungo na dynamic QR yako.
Andika sentensi moja inayouza
Chini ya jina lako, eleza unachomsaidia mteja kufanya. Mfano dhaifu: "Tunauza vifaa vya ofisi." Mfano bora: "Tunasambaza vifaa vya ofisi kwa makampuni Dar es Salaam ndani ya saa 24, kwa ankara rasmi."
Ongeza ushahidi
Picha za kazi halisi, huduma kuu, orodha ya bei au wasifu wa kampuni wa PDF, na ushuhuda wa wateja wawili au watatu. Kila kipengele kinajibu swali ambalo mteja angekuuliza kwenye simu ya kwanza.
Pakua QR na uiweke kwenye muundo wa kuchapisha
Weka QR kwenye kadi za biashara, vipeperushi, brosha, mabango na vifungashio vijavyo. Iandikie mwito wa wazi kama "Scan kuona bei" au "Scan kunihifadhi kwenye simu yako". Kama unachapisha kwetu, tutumie kiungo na tutaiweka kwenye muundo.
Jaribu kabla ya kuchapisha kwa wingi
Chapisha sampuli moja na uiscan kwa simu mbili tofauti, kwa umbali halisi ambao mteja atasimama. QR ya kadi ya biashara isiwe ndogo kuliko sentimita mbili; ya bango iwe kubwa zaidi kulingana na umbali.
Agiza kadi za NFC kwa wanaokutana na wateja
Mameneja, wafanyakazi wa mauzo na timu za maonyesho. Kadi zinachapishwa kwa nembo yako Dar es Salaam, zikiwa na NFC na QR ile ile nyuma. Kwa kampuni, andaa faili la Excel la timu nzima.
Pima kila mwezi na uboreshe
Angalia kadi yako imefunguliwa mara ngapi. Kama idadi haiongezeki baada ya kuweka QR kwenye bango jipya, labda iko juu mno au ni ndogo. Badilisha kitu kimoja, pima mwezi unaofuata.
09Makosa ya kuepuka
Kutumia tovuti ya bure isiyo ya kudumu
Baadhi ya tovuti za bure zinatoa "dynamic QR" inayokufa baada ya majaribio ya siku chache, au inayoonyesha matangazo yao kabla ya ukurasa wako. Kabla ya kuchapisha, hakikisha kiungo ni cha kudumu, QR haina alama ya kampuni nyingine, na hakuna kikomo cha idadi ya wanaoscan. Kwenye DP Card hakuna kikomo cha mara ukurasa unavyofunguliwa, hata kwenye kifurushi cha bure.
QR bila mwito wa kuchukua hatua
QR peke yake haimwambii mteja kwa nini ascan. Andika maneno mafupi kando yake: "Scan kuona bei", "Scan kupata ramani", "Scan kuniongeza".
QR ndogo mno, mahali pabaya, au juu ya rangi isiyotofautiana vya kutosha
QR inahitaji rangi nyeusi juu ya rangi nyeupe au nyepesi, na nafasi tupu kuizunguka. Usiiweke juu ya picha yenye shughuli nyingi, kwenye uso unaong'aa, wala juu mno ya mlango.
Kuchapisha na kusahau
Faida ya dynamic QR ni kubadilika. Weka kumbukumbu kwenye kalenda kila robo mwaka: kagua ukurasa, badilisha picha, bei au ofa.
10Bei za DP Card
Bei zote ziko kwa shilingi na zinajumuisha VAT ya 18%. Malipo ni kwa Mixx by Yas au NMB, kwa ankara rasmi. Bei kamili zinapatikana kwenye ukurasa wa bei.
| Kifurushi | Bei (VAT ndani) | Unachopata |
|---|---|---|
| Bure | TZS 0 | Kadi 1 na QR yake, miundo 3, idadi ya jumla ya mara ilizofunguliwa, bila muda wa mwisho |
| Lite | TZS 11,999 / mwezi TZS 117,999 / mwaka | Kadi 2, miundo yote 20, takwimu za siku 30, msaada wa WhatsApp |
| Pro | TZS 29,999 / mwezi TZS 294,999 / mwaka | Kadi 5, takwimu za siku 90, msaada wa kwanza, bila mstari wa DP chini ya kadi |
| Business | TZS 70,999 / mwezi TZS 707,999 / mwaka | Domain yako, kadi 25 za wafanyakazi, takwimu za mwaka, kupakia kwa Excel, meneja wa akaunti |
| Enterprise | Kuanzia TZS 2,899 / kadi / mwezi | Kwa kampuni zenye wafanyakazi 26 na zaidi: domain yako, kadi za wafanyakazi bila kikomo, ankara ya kampuni |
Uchapishaji wa kadi za NFC, kadi za karatasi, vipeperushi na mabango unapangiwa bei kando kulingana na idadi na muundo. Kwa quotation, wasiliana nasi kupitia WhatsApp +255 711 800 400.
11Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Tofauti kati ya static QR na dynamic QR ni ipi?
Static QR inafungia taarifa ndani yake, hivyo haziwezi kubadilika baada ya kuchapishwa. Dynamic QR inabeba kiungo (link) kisichobadilika kinachoelekeza kwenye ukurasa wako, hivyo unabadilisha ukurasa wakati wowote na QR iliyochapishwa inaendelea kufanya kazi.
Naweza kuweka dynamic QR kwenye kadi za karatasi na vipeperushi?
Ndiyo. Inachapishwa kama picha ya kawaida kwenye kadi za karatasi, vipeperushi, brosha, mabango, magari, vifungashio na risiti.
Kadi ya NFC inahusianaje na dynamic QR?
Kadi ya NFC ni kadi ya plastiki iliyochapishwa yenye chip ya NFC na QR ile ile nyuma. Kugusa au kuscan, zote zinafungua ukurasa mmoja.
Mteja anahitaji app ili kuscan?
Hapana. Kamera za simu janja nyingi zinascan moja kwa moja, na ukurasa unafunguka kwenye browser.
Nikibadilisha namba au anwani, nitachapisha upya?
Hapana. Unahariri ukurasa, na kila QR na kadi ya NFC uliyokwisha kuchapisha inaonyesha taarifa mpya.
Nikichelewa kulipia kifurushi, QR zangu zinakufa?
Hapana. Unapata siku 7 za neema, kisha ukurasa unarudi kwenye kifurushi cha bure. Kiungo na QR vinaendelea kufanya kazi.
Naweza kujua kadi yangu imefunguliwa mara ngapi?
Ndiyo. Unaona mara ngapi kadi yako imefunguliwa, iwe kwa QR, NFC au kiungo, na vifurushi vya kulipia vinaonyesha takwimu za siku 30 hadi mwaka mzima.
Hitimisho
Huhitaji kuacha kadi za karatasi, vipeperushi wala mabango. Unahitaji tu QR ambayo haizeeki pamoja nazo. Dynamic QR inakuruhusu kuchapisha mara moja na kubadilisha taarifa mara nyingi kadiri biashara yako inavyobadilika, huku ukijua kila kitu ulichochapisha kinaleta nini. Kadi ya NFC inaibeba QR hiyo hiyo mkononi mwako kwa mikutano ya ana kwa ana.
Anza na ukurasa wa bure leo. Ndani ya dakika tano utakuwa na QR ya kuweka kwenye muundo wa uchapishaji wako unaofuata.
Pata dynamic QR yako leo
Bure, dakika tano. Kwa uchapishaji wa kadi za NFC, vipeperushi na kadi za biashara zenye QR, tutakuandalia quotation.
Shiriki makala hii
Umewahi kuhudumiwa na DP Promotions?
Maoni yako yanatusaidia kuboresha huduma — na yanawasaidia wengine kutupata.
Asante sana. Ikupendeze, iweke pia Google ili wengine watupate.
Andika review Google