T-Shirt Printing: Mbinu Tofauti na Matokeo Yao
Kuchapisha T-shirt kuna mbinu kadhaa — na kila mbinu ina matokeo, bei, na hali tofauti za matumizi.
Screen Printing
Inatumia wino wa maalum kupitia kichungi kwenye nguo. Inafaa kwa idadi kubwa (MOQ 20+), rangi chache (1-4), na muundo rahisi. Faida: Inakaa muda mrefu, inaonekana mkali.
DTF (Direct to Film)
Inafaa kwa idadi ndogo (hata kipande 1), rangi nyingi, au picha ngumu. Faida: Inaweza kufanya rangi yoyote. Hasara: Inaweza kupasuka baada ya osha nyingi.
Embroidery (Kushona)
Logo inashonwa moja kwa moja kwenye nguo kwa uzi. Inafaa kwa polo shirts na mavazi ya ofisi. Faida: Inaonekana ya hali ya juu sana, inadumu maisha yote ya nguo.
Unafaa Kuchagua Nini?
Uniform ya ofisi: Embroidery. Matukio ya muda mfupi: DTF au Screen. Idadi kubwa: Screen Printing ndiyo bei nafuu zaidi. Washauri wa DP Promotions watakusaidia kuchagua.